Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2019

Mazoezi ya kuondoa kitambi

Picha
Watu wengi wanaotaka kupunguza uzito huamini Kalori ndio kila kitu kinachohusika. Unapochoma Kalori zaidi ya unavyokula, unapunguza uzito. Na kama unakula Kalori nyingi kuzidi mwili wako unavyoweza kuchoma na kutumia, mwili huongeza mafuta. Kinachochoma Kalori mfululizo ni (Lean Muscle Mass) iliyochini ya mafuta ya mwili ambayo huruhusu uchukuaji zaidi wa Kalori bila kuongeza uzito. Mwili hukubaliana na mabadiriko. Kupunguza uzito bila kufanya mazoezi huongeza hatari ya kupoteza (Lean Muscle Mass), kupungua kwa utendaji wa kimetaboliki na kuweka mwili kwenye hali ya kutunza mafuta. MAZOEZI MATANO BORA YA KUONDOA KITAMBI:- 1. THE BICYCLE EXERCISE Lala chali huku mikono yako ikiwa chini ya kichwa chako, leta magoti yako kifuani huku ukinyanyua mabega juu. Taratibu leta kiwiko chako cha kulia hadi kwenye goti la kushoto huku ukinyoosha mguu wako wa kulia. Badili na upande mwingine na ufanye kama unakanyaga pedeli za baiskeli. Fanya zoezi hili seti 1-3 kwa kurudia mara 12-16. ...

Faida za tunda la limao

Picha
Pindi utakapoamua kunywa maji ya limao kwa kila siku asubuhi unaweza ukapata faida zifuatazo; 1.Huongeza Kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo kama mafua, na kikohozi kutokana na kuwa na vitamin C 2. Husafisha Mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia tumbo kujaa gesi mara kwa mara 3. Huleta hewa safi kinywani. Ni Muhimu sana kwa watu wanaonuka midomo 4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana 5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa na ascorbic acid ya kutosha. Pia huimarisha mifupa 6. Husaidia mmeng’enyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umeng’enyaji wa chakula. 7. Himarisha Ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri. 8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha. 9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona. 10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya. Muhimu; kamu...

Faida za tunda Topetope (Stafeli)

Picha
Tope tope ni moja ya tunda ambalo si rahisi sana kulikuta kwenye majokofu ya watu au kwenye orodha ya matunda mara baada ya kula. Pamoja na kwamba tope tope linaladha nzuri na linafaida zake ndani ya mwili, lakini wengi hawalitumii sana hivyo leo nimeona nikupatie hizi faida zake kadhaa huenda zitakufanya uanze kulitumia tunda hili Miongoni mwa faida za tunda hili ni pamoja na hizi zifuatazo:- Tope tope limesheheni vitamin C imbayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na hivyo kumfanya mtumiaji kuepuka kusongwa na magonjwa mara kwa mara. Pia tope tope lina kiasi cha vitami A ambayo hulifanya tunda hilo kuingia kwenye orodha ya matunda yenye uwezo wa kuboresha na kulinda afya ya ngozi na nywele. Aidha, tope tope pia limesheheni madini ya 'potassium', ambayo nayo husaidia miili yetu kuondokana na tatizo la maumivu ya hapa na pale ya mifupa. Kwa wale wenye shida ya maumivu ya mifupa hasa sehemu za maungio 'joint' wanapotumia tunda hili mara kwa ma...

Faida za Kitunguu Swaumu

Picha
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.   Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.   Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.   Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na...

Tunda la Parachichi

Picha
Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.  Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika. Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya. Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika...

Jinsi ya kupunguza mafuta ya mwili bila kufanya mazoezi

Picha
Kama huna muda wa kufanya mazoezi, lishe yako itasaidia sana katika kupunguza mafuta mwilini. Kwa kawaida mwili hutunza wanga kwa njia ya mafuta, kwa hiyo njia rahisi ya kupangilia vyakula vya wanga itasaidia kupunguza mafuta. Njia zifuatazo zitasaidia kupunguza mafuta mwilini. 1. Punguza ulaji wa vyakula vya wanga mwilini. Mboga za majani na matunda huwa na wanga kidogo ukilinganisha na vyakula vya viwandani kama biskuti, chocolates na vyakula vingine jamii ya ngano. 2. Tumia mafuta yatokanayo na mimea katika mapishi. Epuka matumizi ya mafuta yatokanayo na wanyama badala yake tumia mafuta ya alizeti, karanga, nazi na mawese/chikichi. 3. Jaribu kutumia sahani ndogo wakati wa kula ili chakula kionekane kingi na upunguze hamu ya kuongeza chakula. 4. Punguza matumizi ya vinywaji vya wanga kama vile soda na pombe na pia ongeza kiasi cha maji ya kunywa kila siku mpaka kufikia lita tatu kwa siku. Kunywa maji mengi kutasaidia kujihisi kushiba na mwili kua na maji ya kutosha.uu