Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2019

Faida za Tende

Picha
Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipekee. Tunda hili limezoeleka kuliwa wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ila sio mbaya ukapendelea kula.  Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo. Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara. Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi. Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kuji...

Jitibu Maradhi na mmea wa Mlonge

Picha
Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu. Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida zake za kiafya. Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000 ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakam...

Lishe kwa aijili ya watoto wa miezi 6 mpaka 12

Kwa miezi sita ya kwanza katika maisha ya mtoto chakula pekee ambacho wataalamu wa afya wanashauri apewe ni maziwa ya mama tu. Kunyonyesha ndio njia ya kwanza kabisa kumpa mtoto chakula. Unapoanza kumpa mtoto vitu vingine kama maziwa ya kopo wakati ana miezi michache utoaji wako wa maziwa unaathirika maana jinsi mtoto anavyonyonya ndivyo jinsi maziwa yanavyotengenezwa ndio maana watu wengi wanavyoanza kazi na kumuacha mtoto nyumbani maziwa yao yanaanza kupungua. Faida za kunyonyesha maziwa ya mama ni pamoja na: Maziwa ya mama yana virutubisho vingi vya asili ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji na kinga kwa mtoto. Humlinda na magonjwa mengi ya utoto pamoja na ‘allergies’ mbalimbali. Hukuwezesha kuwa na ukaribu na mtoto wako. Hukupunguzia uwezekano wa kupata kansa ya matiti. Ni bure na unaweza kumpatia maziwa wakati wowote bila usumbufu. Wakati gani Uanze Vyakula Vingine Mtoto wako akifikisha miezi 6 unaweza kuanza kumpatia vyakula vingine kidogo kidogo ( Kuna ambao kutokana ...